Maradhi ya kipindupindu yakumba kaunti ya Tana River

Maradhi ya kipindupindu yakumba kaunti ya Tana River

by -
0 318

Idara ya afya kaunti ya Tana River inasema zaidi ya watu 20 wamepimwa na kugunduliwa na maradhi ya kipindupindu eneo la Tana Delta kaunti hiyo.

Idadi ya waathiriwa imefikia zaidi ya 20 baada ya ugonjwa huo kuzuka wiki jana.

Watu 8 walifariki mapema wiki hii eneo hilo la Tana Delta kutokana na maradhi hayo.

Afisa mkuu wa afya kaunti hiyo Hassan Komoro ameambia Baraka Fm kwamba wanaendelea na kuchukua hatua za kuepuka maambukizi zaidi.

Kulingana na Komoro, walioambukizwa wametengewa sehemu maalum wanakotibiwa katika eneo la Kibusu kaunti ndogo ya Tana Delta ili kuzuia maambukizi zaidi.

Amesema wanasaidiana na shirika la msalaba mwekundu na mamlaka ya kupambana na majanga nchini NDMA kudhibiti hali.

Afisa wa matibabu katika hospitali ya Ngao iliyo Tana Delta Nicholas Mwenda amedokeza mashirika hayo yamesaidia kupata dawa kutoka kwa vituo vingine vya afya ili kudhibiti hali hiyo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES