Simon Sang achaguliwa tena kuongoza makuli bandarini

Simon Sang achaguliwa tena kuongoza makuli bandarini

by -
0 361
Simon Sang achaguliwa tena kwa muhula wa tatu

Mombasa, KENYA: Simon Sang amechaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa muungano wa makuli bandarini yaani Dock Workers Union.

Hii ni kufuatia uchaguzi uliofanyika Jumanne kuchagua viongozi wapya wa muungano huo.

Matokeo yametangazwa mapema Jumatano.

Sang ambaye sasa amechaguliwa kuhudumu kwa muhula wa tatu, ameahidi kupigania haki za wafanyakazi bandarini ili kuepuka migomo ya mara kwa mara .

Pia ameahidi kuzindua manifesto ya sera ya muungano wa makuli itakayotoa mwongozo wa miaka mitano au zaidi.

“Sisi hatupendi strike, lakini pia hatupendi kudhulumiwa. We have been misunderstood for the last five years. We must be understood this time round. Na jukumu langu la kwanza kabla sijarudi CBA next week, litakuwa ni Dock Workers Union tuonane na mkubwa wa serikali ambaye ni president Uhuru Kenyatta.” Amesema Sang baada ya kutangazwa mshindi.

Anthony Olonde amechaguliwa kuwa naibu katibu mkuu.

Mohamed Sheria amechaguliwa mwenyekiti huku Gunda Kaneno akichaguliwa kuwa naibu mwenyekiti.

Muungano huo wa makuli bandarini hutetea maslahi ya wafanyakazi bandarini.

 

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES