Makuli bandarini Mombasa wapiga kura

Makuli bandarini Mombasa wapiga kura

by -
0 391
Simon Sang anayewania wadhifa wa ukatibu kwa muhula wa tatu

Mombasa, KENYA: Muungano wa makuli bandarini yaani Dock workers Union kinafanya uchaguzi hivi leo kuchagua viongozi wapya.

Wanachagua katibu mkuu, naibu wake, mwenyekiti na naibu wake, miongoni mwa viongozi wengine.

Makuli wapatao elfu 5 wanatarajiwa kupiga kura.

Katibu wa sasa Simon Sang anawania nafasi hiyo kwa muhula wa tatu.

Sang anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Katana Wara ambaye ni mdhamini wa mpango wa malipo ya uzeeni katika mamlaka ya bandari nchini KPA, Bakari Bweta ambaye ni katibu wa zamani wa muungano wa wafanyakazi na pia mkurugenzi wa zamani wa KPA Abdalla Randani.

Mwenyekiti Geoffrey Mareko anasema Sang na kikosi chake wamekuwa wakipanga kuiba kura.

Muungano huo wa makuli bandarini hutetea wafanyakazi na kushinikiza mazingira bora ya kufanyia kazi katika bandari ya Mombasa.

Baraka Fm imebaini kuwa baadhi ya wafanyakazi wa bandarini walioachishwa kazi hapo awali wanawania nafasi katika uchaguzi huo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES