Bunge la Jumuiya ya Afrika ya mashariki lazuru Taita-Taveta

Bunge la Jumuiya ya Afrika ya mashariki lazuru Taita-Taveta

by -
0 332

Wajumbe wa bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki wamezuru kaunti ya Taita Taveta, kukutana na viongozi pamoja na wafanyabiashara wa eneo hilo.

Wajumbe hao wamejadili jinsi ya kuboresha biashara kati ya mataifa wanachama.

Anisa Sanguli, mbunge mteule katika bunge la kaunti ya Taita Taveta ameomba wabunge wa Jumuiya hiyo kubuni sheria zitakazorahisisha biashara baina ya mataifa wanachama.

Anisa amesema wafanyabiashara kutoka humu nchini hunyanyaswa katika mataifa mengine jirani, hivyo kuna haja ya kukabiliana na hali hiyo.

Naye mbunge wa jumuiya hiyo Nancy Abisa amehakikishia wafanyabishara kuwa wako katika mikakati ya kuhakikisha kuna soko huru baina ya mataifa wanachama.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES