Aliyerarua nguo za mpenzi wake kukaa jela

Aliyerarua nguo za mpenzi wake kukaa jela

by -
0 457

Mombasa,KENYA:Mwanamume mmoja amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani na mahakama ya Mombasa kwa kosa la kurarua nguo za mpenzi wake pamoja na kumwibia simu.

Mahakama iliambiwa kuwa Billy Omwangala Anyanzwa, aliingia kwa chumba cha mpenzi wake Eunice Njeri eneo la Kaa Chonjo –Tudor na kurarua nguo zake zenye thamani zaidi ya shilingi elfu 30 na simu ya mkono huku akitishia kumpiga.

Mshtakiwa alikubali mashtaka na kuiambia mahakama alikuwa na hasira na mpenzi wake akimshuku kuwa ana mpango wa kando.

Hukumu ilitolewa na hakimu Diana Mochache.

Wakati huo huo mwanamume mmoja ameshtakiwa katika mahakama hiyo kwa madai ya ubakaji.

Sudi Hassan Juma anadaiwa kubaka msichana wa umri wa miaka 13 tarehe 31 mwezi wa Octoba mwaka 2015 katika eneo la Likoni.

Mshukiwa alikana shtaka na hakimu Irene Ruguru akaagizia aachiliwe kwa dhamana ya shilingi laki mbili.

Kesi itasikizwa tarehe 16 mwezi wa Mei.

Comments

comments