MCA wa Shanzu aitaka mahakama iharakishe kesi inayomkabili

MCA wa Shanzu aitaka mahakama iharakishe kesi inayomkabili

by -
0 377
MCA wa Shanzu Maimuna Mwawasi akiwa kotini Mombasa. PICHA: HISANI

Mwakilishi wa wadi ya Shanzu Maimuna Salim Mwawasi anaitaka mahakama ya Mombasa  kusikiliza na kuamua kwa haraka kesi ya ufisadi inayomkabili.

Maimuna anataka kesi hiyo isikilizwe na kuamuliwa kabla ya uchanguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2017.

Kupitia wakili wake Oduory Simiyu, Maimuna ameiomba mahakama kuharakisha kesi hiyo ili apate fursa ya kugombea kiti cha uwakilishi wa wadi wa Shanzu.

Hayo yamejiri baada ya hakimu Susan Shitubi kuahirisha  kesi hiyo iliyotarajiwa kusikizwa Jumatatu akisema ni kwa sababu zisizoweza kuepukika.

Maimuna anadaiwa kupokea hongo ya shilingi Milioni 1.5 kutoka kwa Leah Morin Aketch ili kutatua mzozo wa ardhi baina ya yake na kaunti ya Mombasa mnamo Julai mwaka  jana.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 26 mwezi Aprili.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES