Hofu ya athari za mvua yaibuka miongoni mwa wakaazi wa mitaa duni

Hofu ya athari za mvua yaibuka miongoni mwa wakaazi wa mitaa duni

by -
0 317

Mombasa, KENYA: Wakaazi wa mitaa duni kaunti ya Mombasa wanahofia huenda wakaathirika endapo mvua iliyoanza kunyesha itazidi.

Waliozungumza na Baraka Fm wanasema wana wasiwasi kuhusiana na mikakati ya kukabiliana na majanga.

Wanahisi bado serikali ya Mombasa haijafanya juhudi zifaazo kukabiliana na majanga.

Maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha Jumapili Mombasa, tayari yameathiri mitaa kadhaa na pia barabara katika maeneo mbalimbali ya Mombasa.

Lakini shirika la msalaba mwekundu wiki jana, lilianza kutoa hamasa kwa umma kuhusu kukabiliana na majanga yanapotokea likilenga mitaa duni ya Mburu Kenge na Moroto Tudor, Bangladesh huko Changamwe na sehemu zingine.

Hayo yakijiri wakaazi wa Chanzou wadi ya Chengoni – Samburu kaunti ya Kwale wanalalamikia hali mbaya ya barabara eneo hilo hasa wakati huu ambapo msimu wa mvua umeanza.

Wenyeji hao wanasema kuna umuhimu wa kuweka daraja katika mto wa Kwa Nzile ambao kwa sasa umefurika na kuvunja kingo zake hali inayotatiza usafiri katika eneo hilo.

Pia wanasema masomo hukatizwa wakati wa mvua kubwa kwani wanafunzi hushindwa kuvuka mto huo kufuatia mafuriko.

Sasa wanalaumu serikali ya kaunti ya Kwale wakisema haijatekeleza ahadi yake iliyotoa hapo awali ya kuweka daraja katika mto huo.

Taarifa zaidi kutoka kwa Laurence Sita

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES