Wadaiwa kumbaka msichana mdogo na kumwambukiza virusi vya H.I.V.

Wadaiwa kumbaka msichana mdogo na kumwambukiza virusi vya H.I.V.

by -
0 287

Wanaume  wanne wamefikishwa mahakamani  Mombasa  kwa madai ya kumbaka msichana wa umri mdogo na kumwambukiza virusi vya H.I.V. vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi.

Isaac Musembi, Komu Muthini, Onesmus Mbuvi na Mutingo Kimeu wanadaiwa kumbaka msichana wa umri wa miaka 10 na kumwambukiza virusi hivyo kati ya mwezi Septemba mwaka jana na mwezi April mwaka huu katika mtaa wa mabanda wa Moroto hapa Mombasa.

Mahakama imeambiwa msichana huyo wa darasa la nne alimweleza afisa wa usalama kuwa anawafahamu vyema washukiwa na walimdanganya kwa kutumia peremende, pesa na pia walimuonesha video za ngono kutumia simu ya mkononi kabla ya kumbaka.

Afisa wa upelelezi katika kituo cha polisi cha Makupa Joyce Okemo amewasilisha ombi la kutaka washukiwa wasiachiwe kwa dhamana akisema wangeweza kuadhibiwa na raia waliokuwa na hasira.

Bi. Joyce pia ameiomba mahakama iruhusu washukiwa kupelekwa katika hospitali ya Coast General kupimwa hali yao ya kiafya kuhusiana na virusi vya HIV.

Pia ameomba muda wa wiki moja kuwawezesha kukamilsha uchunguzi na pia kuandaa ripoti ya daktari.

Hakimu Susan Shitubi ameagiza washukiwa kuregeshwa mahakamani Alhamisi ijayo kusomewa mashtaka.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES