Usajili wa wapiga kura Malindi, Lamu na Kericho kuanza

Usajili wa wapiga kura Malindi, Lamu na Kericho kuanza

by -
0 327

Nairobi, KENYA:Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inasema usajili wa wapiga kaunti ya Lamu, eneo bunge la Malindi na kaunti ya Kericho utaanza rasmi tarehe 18 mwezi aprili mwaka huu.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari tume hiyo imesema zoezi hilo litaendelea  hadi tarehe 17 mwezi Mei.

Usajili wa wapiga kura katika eneo bunge la  Malindi  na kaunti ya Kericho haukuendelea mwezi wa februari kutokana na uchaguzi mdogo uliokuwa ukiendelea maeneo hayo.

Katika kaunti ya Lamu zoezi hilo lilisitishwa  kutokana na masuala tatanishi ya kisheria.

IEBC inasema makarani 182 watafanikisha zoezi hilo katika maeneo hayo, na inalenga kusajili zaidi ya wapiga kura laki 100 katika maeneo hayo matatu.

Imehaririwa na Joseph Jira

Comments

comments