Washukiwa wa alshabab washtakiwa mahakamani Mombasa

Washukiwa wa alshabab washtakiwa mahakamani Mombasa

by -
0 339

Mombasa,KENYA:Vijana wanne wemeshtakiwa katika mahakama Mombasa kwa madai ya kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la al-shabaab.

Kassim Ahmed, Ali Omar, Mohamed Kassim na Mustafa Kheri wanadaiwa kuwa wanachama wa kundi hilo na pia kumiliki bunduki aina ya G3 na risasi kadhaa kinyume na sheria.

Mahakama imeambiwa kuwa washukiwa hao walipatikana kwa nyumba moja eneo la Majengo mwezi Januari.

Lakini wamekana mashtaka yanayowakabili mbele ya hakimu Susan Shitubi.

Washukiwa hao wanakabiliwa na kesi nyingine katika mahakama tofauti itakayosikilizwa mwezi Julai tarehe 27.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES