Polisi Mombasa kuzuru eneo alikopigwa risasi kijana

Polisi Mombasa kuzuru eneo alikopigwa risasi kijana

by -
0 347

Mombasa,KENYA:Wakuu wa polisi mjini Mombasa pamoja na wakuu wa ujasusi watazuru eneo la Shonda huko Likoni ambako kijana mmoja anadaiwa kupigwa risasi na afisa wa polisi kimaksudi.

Familia ya kijana huyo inadai mwanao alipigwa risasi na afisa wa polisi anayehudumu eneo la likoni walipokuwa wakishika doria.

Familia hiyo inadai kuwa afisa huyo alikuwa na nia ya kumwuua kijana huyo.

Hata hivyo naibu mkuu wa polisi wilayani Likoni Anthony Shimoli alikana tukio hilo na akiwatetea maafisa hao wa polisi.

Shimoli aliwataka walio na ushahidi kuhusu madai hayo kuandikisha taarifa kwa polisi.

Imehaririwa na Joseph Jira

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES