ICC yatupilia mbali kesi dhidi ya Ruto na Sang

ICC yatupilia mbali kesi dhidi ya Ruto na Sang

by -
0 465
Ruto (kushoto) na Sang (Kulia)

Hague, UHOLANZI: Mahakama ya kimataifa kuhusu kesi za uhalifu wa kivita ICC huko Uholanzi imetupilia mbali kesi iliyokuwa ikiwakabili naibu wa rais Wiliam Ruto na aliyekuwa mwanahabari Joshua Sang katika mahakama hiyo.

Hii ina maana Ruto na Sang hawana kesi ya kujibu dhidi ya madai ya kuchochea ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.

Majaji wa ICC wamesema upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashtaka.

Awali, majaji wa ICC walifutilia mbali ombi la kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda la kutaka mahakama itumie ushahidi wa mashahidi waliobadilisha nia.

Haya yanakuja baada ya mahakama hiyo ya ICC mwezi Disemba mwaka jana kutupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili rais Uhuru Kenyatta katika mahakama hiyo.

Majaji hao pia walisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumfungulia rais Kenyatta mashtaka.

Hii ina maana washukiwa wote sita wa humu nchini waliodaiwa kuchochea ghasia za uchaguzi wa mwaka wa 2007 wameondolewa mashtaka.

Wengine waliotajwa na kuondolewa mashtaka hapo awali ni aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura, waziri wa zamani Henry Kosgey na aliyekuwa kamishna wa polisi Hussein Ali.

Wote walidaiwa kuchochea ghasia hizo za uchaguzi wa mwaka 2007 zilizoendelea hadi mwaka wa 2008.

Watu takriban 1,200 waliuawa wakati wa mapigano hayo.

 

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES