Polisi wamsaka mlanguzi wa binadamu Kwale

Polisi wamsaka mlanguzi wa binadamu Kwale

by -
0 373

Kwale,KENYA:Polisi huko Kwale wanamsaka mtu anayedaiwa kuwa mlanguzi wa binadamu.

Mtu huyo ambaye polisi wamemtaja kwa jina “Chengo”, anasemekana amekua akiwapa hifadhi raia wa kigeni waliongia humu nchini kinyume cha sheria.

Anadaiwa kutoroka baada ya kupata habari kuwa anasakwa na polisi muda baada ya raia wa kigeni kufumaniwa maeneo ya Lungalunga.

Hayo yanajiri huku raia 13 wa Ethiopia kukamatwa Lungalunga wiki jana.

OCPD wa Msambweni Joseph Omijah amesema raia hao walikuwa wamejifisha vichakani.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES