Kijana aaga dunia akijaribu kujiunga na idara ya polisi

Kijana aaga dunia akijaribu kujiunga na idara ya polisi

by -
0 531

Kwale, KENYA: Kijana amefariki alipokuwa akishiriki zoezi la kusajili makurutu wa kujiunga na idara ya polisi huko Matuga kaunti ya Kwale.

Mwarika Mwalimu wa umri wa miaka 23, ameanguka na kuzirai wakati wa majaribio kabla ya kuthibitishwa kufariki katika hospitali ya Kwale.

Ripoti ya daktari kutoka hospitali hiyo inasema huenda amefariki baada ya msukumo wa damu kufeli mwilini.

Afisa mkuu wa polisi anayesimamia zoezi hilo kaunti ndogo ya Matuga Moses Awiti anasema kijana huyo alikamilisha mbio za majaribio za kilomita 6 na kufaulu mchujo wa kwanza pamoja na vijana wengine 38.

Zoezi hilo la kusajili makurutu watakaojiunga na idara ya polisi limefanyika Jumatatu katika maeneo mbali mbali nchini.

Mjini Mombasa vijana 10 eneo la Mvita wameteuliwa kujiunga na kikosi cha polisi wa utawala huku 20 wakijiunga na kikosi cha polisi wa kawaida.

Kamishna wa tume ya huduma kwa polisi Murshid Mohammed anasema ukaguzi zaidi utafanywa ambapo itachukua muda wa majuma mawili kubaini makurutu ambao watafaulu kujiunga na idara ya polisi.

Taarifa zaidi kutoka kwa Weldon Kemboi

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES