Wahamiaji haramu wakamatwa Kwale

Wahamiaji haramu wakamatwa Kwale

by -
0 308

Kwale,KENYA:Polisi kaunti ya Kwale inasema imewakamata washukiwa 13 wa uhamiaji haramu raia wa Ethiopia, katika eneo la Majoreni-Lungalunga wakiwa wamefichwa msituni.

Polisi wanasema washukiwa hao walikuwa safarini kuelekea Afrika Kusini kupitia nchi jirani ya Tanzania.

Mkuu wa polisi eneo hilo Joseph Omijah amesema watu hao hawakuwa na stakabadhi zozote za kujitambulisha na polisi wanamsaka wakala anayedaiwa kuendesha biashara ya ulanguzi wa binaadam.

Omijah amesema washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Diani na watafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.

Comments

comments