Polisi yaimarisha usalama katika vyuo na taasisi Pwani

Polisi yaimarisha usalama katika vyuo na taasisi Pwani

by -
0 267

Mombasa,KENYA: Idara ya usalama ukanda wa pwani inasema imeimarisha usalama katika taasisi na vyuo vyote kutokana na tishio la ugaidi.

Vyuo hivyo ni pamoja na chuo cha kiufundi cha Technical University of Mombasa-TUM, na taasisi  ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea taaluma ya udaktari mjini Mombasa KMTC.

Afisa mmoja wa polisi ameiambia Baraka fm kuwa idara ya usalama imeongeza idadi ya maafisa wa polisi wanaolinda taasisi hizo tofauti na awali.

Kumekuwa na taaarifa kuwa huenda wanamgambo wa alshabaab wanapanga kutekeleza mashambulizi katika vyuo hivyo.

Zaidi ya maafisa 20  wa usalama sasa wanalinda vyuo hivyo tofauti na awali ambapo walikuwa ni maafisa 5 pekee.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES