Kesi dhidi ya Mishi Mboko yaendelea mahakamani Mombasa

Kesi dhidi ya Mishi Mboko yaendelea mahakamani Mombasa

by -
0 353

Mombasa, KENYA: Kesi ya uchochezi dhidi ya mwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Mishi Juma Mboko imeendelea mahakamani Mombasa huku shahidi wa kwanza akiitwa kutoa ushahidi.

Shahidi huyo ametoa nakala ya video mbele ya mahakama iliyorekodiwa siku ya madaraka day mwaka wa 2014 ambapo Mishi Mboko anadaiwa kutamka matamshi ya chuki na ukabila.

Mahakama pia imeagiza mashahidi wanne waliokataa kufika mahakamani kwa madai ya kutishwa na upande wa mshtakiwa kufikishwa mbele ya mahakama  tarehe 12 mwezi Mei.

Upande wa mashtaka umeambia mahakama kuna mashahidi 6 katika kesi hiyo.

Shahidi wa pili ambaye ni afisa mpelelezi alianza kutoa ushahidi lakini akazuiwa na upande wa mashtaka baada ya kusema hakuwa na kamera iliyo rekodi video hiyo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES