Msichana akiri kumwekea mwanamume dawa kabla ya kumwibia

Msichana akiri kumwekea mwanamume dawa kabla ya kumwibia

by -
0 318

Mombasa, KENYA: Msichana amekiri mbele ya mahakama ya Mombasa, kumwekea mwanamume dawa ya kumpoteza fahamu kabla ya kumwibia mali.

Mary Wanjiru wa umri wa miaka 17, amekiri shtaka la kumpa Kevin Gathenya dawa aina ya nohypol iliyompoteza fahamu na kisha kumwibia mali nyumbani kwake.

Mary alidaiwa kuiba mali ya thamani ya zaidi ya shilingi laki tatu nyumbani kwa Kevin eneo la Tudor mjini Mombasa baada ya mwanamume huyo kupoteza fahamu.

Mshukiwa alitoweka baada ya kutekeleza wizi lakini akakamatwa wiki jana eneo la Mariakani.

Hakimu Susan Shitubi ameagiza msichana huyo apelekwe hospitali ya Coast General kwa uchunguzi wa kuthibitisha umri wake kabla ya kuhukumiwa.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES