Maelfu bado waugua kipindupindu nchini

Maelfu bado waugua kipindupindu nchini

by -
0 313
Muathiriwa wa ugonjwa wa kipindupindu. PICHA: HISANI

Nairobi, KENYA: Watu wapatao 216 wamefariki kufikia sasa huku wengine elfu 13 wakilazwa hospitali kutokana na ugonjwa wa kipindupindu tangu ugonjwa huo uzuke mwaka 2014 humu nchini.

Wizara ya kitaifa ya afya inasema kaunti 12 zinaripoti visa vya ugonjwa huo wa kipindupindu kwa sasa japo inasema kaunti 16 zimefanikiwa kukabiliana na maradhi hayo.

Wizara hiyo hata hivyo inasubiriwa kutoa takwimu za vifo na waliolazwa hospitali kutokana na kipindupindu tangu mwezi Januari.

Katibu katika wizara ya afya Nicholas Muraguri anasema kaunti kadhaa zimeripoti kipindupindu kwa mara ya kwanza tangu ugonjwa huo uzuke mwaka 2014.

Miongoni mwazo ni kaunti ya Tana River iliyo Pwani, Wajir, Marsabit, Tharaka Nithi, Meru, Busia na Nandi.

Muraguri hata hivyo anasema kaunti nyingi zimejizatiti kukabiliana na maambukizi ya maradhi hayo hasa kwa kudumisha usafi.

Maradhi ya kipindupindu aghalabu husababishwa na mazingira machafu.

Comments

comments