Kaunti ya Mombasa yasema imejiandaa kukabili Kipindupindu

Kaunti ya Mombasa yasema imejiandaa kukabili Kipindupindu

by -
0 278

Mombasa, KENYA: Serikali ya kaunti ya Mombasa inatoa hakikisho kuwa imejiandaa vilivyo kukabili maradhi ya kipindupindu endapo yatazuka tena mjini Mombasa kama inavyoripotiwa katika maeneo mengine nchini.

Waziri wa afya kaunti ya Mombasa Mohammed Abdi anasema serikali ya Mombasa imejiandaa kuhakikisha yeyote atakayepatikana na dalili za maradhi hayo anatibiwa haraka.

Hatua hii inajiri wakati Idara ya afya nchini ikitoa tahadhari kuhusu maradhi hayo ya kipindupindu.

Kulingana na wizara ya kitaifa ya afya, watu 216 wamefariki na wengine elfu 13 kulazwa hospitali kutokana na ugonjwa wa kipindupindu tangu ugonjwa huo uzuke mwaka 2014.

Katibu katika wizara ya kitaifa ya afya Nicholas Muraguri anasema kaunti kadhaa zimeripoti kipindupindu kwa mara ya kwanza tangu ugonjwa huo uzuke mwaka 2014, miongoni mwazo kaunti ya Tana River iliyo eneo la Pwani.

Kaunti zingine ni Wajir, Marsabit, Tharaka Nithi, Meru, Busia na Nandi.

 

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES