Balala atathmini kuondoa marufuku ya watalii kuzuru Lamu

Balala atathmini kuondoa marufuku ya watalii kuzuru Lamu

by -
0 398
Waziri wa utalii Najib Balala(katikati) akiwa na viongozi wengine alipozuru kaunti ya lamu.

Lamu, KENYA: Waziri wa Utalii Najib Balala anatathmini kuhusu namna ya kuondoa marufuku iliyowekwa dhidi ya watalii kuzuru kaunti ya Lamu.

Waziri Balala alisema  wizara yake inajitahidi kuondoa marufuku hiyo iliyodumu kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Alisema serikali yake imepiga hatua kuhakikisha usalama unadumishwa kaunti hiyo ya Lamu.

Waziri huyo alisema usalama mjini Lamu umeimarika  pakubwa ikilinganishwa na miaka miwili nyuma ambapo kulishuhudiwa utovu wa usalama  na kusababisha watu wapatao 100 kuuawa.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES