Sehemu zilizoshuhudia uvamizi Lamu zafikiwa na huduma ya mawasiliano

Sehemu zilizoshuhudia uvamizi Lamu zafikiwa na huduma ya mawasiliano

by -
0 265

Serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na kampuni za mawasiliano nchini imekamilisha ujenzi wa minara mitatu mikuu ya mawasiliano katika maeneo ambayo yalishuhudia uvamizi wa mara kwa mara kutoka kwa kundi la kigaidi la al-shabaab katika  Kaunti ya Lamu.

Maeneo hayo ni Pandanguo, Mangai, Bodhei.

Zaidi ya wakaazi elfu 3 wanaoishi katika maeneo hayo sasa wanaweza kuwasiliana kutumia yasimu za mkononi huduma ambayo hawajakuwa wakiipata.

Serikali ya kitaifa iliafikia hatua ya kujenga minara hiyo ya mawasiliano katika sehemu hizo kama hatua ya kuimarisha mawasiliano baina ya wananchi na  walinda usalama.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES