Zainab Chidzuga kupambana na gavana wa Kwale 2017

Zainab Chidzuga kupambana na gavana wa Kwale 2017

by -
0 1512
Mwakilishi wa Wanawake kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga ambaye ametangaza azma ya kugombea ugavana mwaka 2017. PICHA:HISANI

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga ametangaza rasmi azma ya kuwania kiti cha ugavana wa kaunti hiyo mwaka 2017.

Tangazo la Chidzuga linakuja baada ya balozi anayewakilisha Kenya nchini Tanzania Ali Chirau Mwakwere kutangaza nia ya kuwania ugavana wa kaunti hiyo katika uchaguzi ujao.

Chidzuga anakosoa uongozi wa Gavana wa sasa wa Kwale Salim Mvurya akisema ameshindwa kukabili ufisad Kwale.

Mwakilishi huyo wa wanawake anasema ametosha kuwania kiti hicho na kwamba ana matumaini ya kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.

Haya yanajiri siku chache baada yake kutangaza kukihama chama cha ODM kilichomplekea bungeni.

Akitoa sababu ya kuhama,bi Chidzuga alidai kuwa ODM ilidinda kumsaidia kuchangisha pesa za kuwasaidia wanawake katika kaunti yake.

Alisema tofauti na ODM, muungano tawala wa Jubilee ulimsaidia, hivyo ataendelea kufanyakazi pamoja nao na wala sio upinzani.

Taarifa zaidi na George Otieno

Comments

comments