Washukiwa wa mauaji ya Mpeketoni, Lamu kujibu mashtaka

Washukiwa wa mauaji ya Mpeketoni, Lamu kujibu mashtaka

by -
0 333

MOMBASA, KENYA: Mahakama kuu mjini Mombasa imewapata na kesi ya kujibu watu wawili walioshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya kigaidi huko Mpeketoni kaunti ya Lamu mwaka wa 2014.

Jaji Martin Muya amesema upande wa mashtaka umetoa ushahidi wa kuonesha kwamba washukiwa hao wanastahili kujibu mashtaka.

Washukiwa Diana Salim na Mahdi Swaleh wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya watu wengi, huko Mpeketoni kaunti ya Lamu.

Mahdi Swaleh ambaye ni mfanyibiashara na Diana Salim ambaye ni Dereva wamekuwa nje kwa dhamana wakati kesi hiyo ikiskizwa kuhusiana na mauaji ya watu zaidi ya 60.

Comments

comments