Serena, Djokovic, Wafuzu Fainali ya Australia Open.

Serena, Djokovic, Wafuzu Fainali ya Australia Open.

by -
0 367
Serena akijaribu kutetea ubingwa wa tennis katika mashindano ya Australia Open mjini Melbourne.

MELBOURNE: Serena Williams wa Marekani amedhihirisha kuwa yeye ndiye nyota hodari zaidi duniani katika tennis ya wanawake, na huenda akazidi kutawala kwa miaka mingi zaidi.

Mapema Alhamisi Serena alifuzu kwa fainali ya mashindano ya Australia Open yanayoendelea mjini Melbourne huko Australia, kwa kumshinda Agnieska Radwanska wa Poland seti za seti mbii za (6-4,6-0) katika mchezo uliochukua dakika 64.

Katika nusu-fainali ya pili matumaini ya Johanna Konta wa Uingereza yalikatizwa pale alipofungwa na Angelique Kerber wa Ujerumani, ambaye sasa atakutana na Serena katika fainali mapema Jumamosi.

Alhamisi pia ilishuhudia Novak Djokovic wa Serbia akimshinda mpinzani wa miaka mingi Roger Federer wa Switzerland seti za ( 6-1, 6-2, 3-6 na 6-3 ) na kufuzu kwa fainali ya wanaume katika Australia Open.

Djokovic atacheza katika fainali dhdi ya Andy Murray wa Uingereza au Milos Raonic wa Canada.

Comments

comments