Sera ya kukabili ugaidi kuzinduliwa na serikali

Sera ya kukabili ugaidi kuzinduliwa na serikali

by -
0 231

NAIROBI, KENYA: Serikali inasema imekaribia kuzindua sera itakayosaidia kukubaliana na ugaidi na mafunzo ya itikadi .

Mkutano tayari umefanyika mjini Nairobi uliowaleta pamoja mabalozi, vyombo vya usalama, viongozi wa kidini na maafisa wa kituo cha kukabili ugaidi humu nchini kuweka mikakati ya kubuni sera hiyo.

Katika mkutano huo imebainika kuwa idadi ya vijana ambao wanajisalimisha kutoka kwa makundi ya kigaidi inaridhisha.

Wadau waliokutana wanaziomba serikali za kaunti kusaidia vijana kujinasua kutoka kwa ugaidi kwa kubuni nafasi zaidi za ajira .

Comments

comments