Fisi mla watu auawa Tana-Delta.

Fisi mla watu auawa Tana-Delta.

by -
0 894
Fisi huyu alipigwa picha akipanua kinywa chake kupiga miayo, ishara ya kubanwa na njaa.

HOLA, KENYA: Wanakijiji waliokuwa na hasira Jumanne walimuua fisi msumbufu eneo la Tana Delta kaunti ya Tana River, baada ya fisi huyo kumuua mtoto wa umri wa miaka miwili.

Ripoti zinasema kuwa fisi huyo alinaswa kwa mtego uliowekwa na maafisa wa shirika la uhifadhi wanyama-pori, kabla ya wanakijiji kumpiga hadi kufa.

Maafisa wa shirika la KWS eneo hilo walidhibitisha kupokea habari kuhusu mtoto aliyeripotiwa kuuawa na fisi, na mtoto mwingine aliyejeruhiwa.

Mnyama huyo msumbufu alikuwa amezua hofu miongoni mwa watu sehemu hiyo ya Tana Delta, na zaidi kuwatisha watoto ambao wengi walikatiza kwenda shule wakohifia kushambuliwa njiani.

Comments

comments