CORD itaendelea kutamba pwani, asema Raila Odinga

CORD itaendelea kutamba pwani, asema Raila Odinga

by -
0 586

Muungano wa CORD unasisitiza kuwa utasalia kuwa imara katika eneo la pwani licha ya juhudi za viongozi wengine kujaribu kuumaliza kisiasa.

Akizungumza mjini Mombasa, kiongozi wa CORD Raila Odinga amekosoa viongozi wa muungano wa Jubilee kwa kujaribu kutumia mbinu zisizofaa kuwarai viongozi wa CORD kuhamia Jubilee.

Raila amesema pwani italasia kuwa ngome ya CORD na kueleza matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi mapema mwezi Machi.

Akigusia yaliyotokea wakati wa ziara ya rais Uhuru Kenyatta eneo la pwani, Raila amekosoa ziara hiyo akidai Jubilee haina nia ya kuleta maendeleo kwani imekuwa ikitoa ahadi za uongo.

“Hawa jamaa wameshindwa, waliahidi watapeana ajira kwa vijana..vijana mmepata ajira? Walisema eti wataleta laptop kwa shule…. Haya yote yalikuwa ni yale madebe matupu kama kunyamba kwa punda…”

Raila amemshtumu Seneta wa Nairobi Mike Sonko kwa kujaribu kushukisha hadhi ya Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho wakati wa ziara hiyo ya rais.

Amesema ni aibu kwa kiongozi kutamka maneno ya matusi mbele ya rais kwa malengo yake ya kibinafsi.

Hata hivyo Raila amempongeza Gavana wa Mombasa Hassan Joho kwa kusalia imara kupeperusha bendera ya CORD.

Amesihi vijana kuungana na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo pwani na kwa taifa pia.

Raila amewaambia wapwani kukataa kupotoshwa na wanasiasa walio na nia mbaya.

Alikuwa akizungumza wakati wa kuzindua rasmi barabara iliyopewa jina la marehemu mwanawe Fidel Odinga eneo la Nyali kaunti ya Mombasa.

Comments

comments