Waziri Wa Marekani Jewell Ashauri Kuhusu Ujangili

Waziri Wa Marekani Jewell Ashauri Kuhusu Ujangili

by -
0 415

Kenya yaendelea kushuhudia bidhaa za magendo zikiingizwa nchini kupitia bandari ya Mombasa.

Kutoka kushoto ni gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, waziri wa mazingira Kenya Judy Wakhungu, waziri wa mambo ya ndani Marekani Sally Jewell, balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec, na mkurugenzi wa mamlaka ya KPA Gichiri Ndua.
Mombasa, Kenya: Waziri wa maswala ya ndani katika serikali ya Marekani Bi Sally Jewell anayezuru Kenya ametia sahihi mkataba wa makubaliano na serikali ya Kenya katika vita dhidi ya uwindaji haramu unaoripotiwa katika mataifa mengi barani Afrika.
 
Bi Jewell amesema serikali ya Marekani imejitolea kusaidia Kenya sawa na nchi zingine kukabili uovu wa kuangamiza wanyama, katika harakati za kulinda mazingira.
 
Akiwa katika bandari ya Mombasa Jumanne mchana waziri Jewell alisema nchi hizo mbili zimekubaliana azimio la kuzuia baishara haramu kama vile dawa za kulevya, pemba za ndovu, na bidhaa haramu zinazopitishwa katika bandari.
 
Katiza ziara hiyo waziri Sally Jewell aliandamana na balozi wa Marekani nchni Kenya Robert Godec, pamoja na waziri wa mazingira nchini Kenya Bi. Judy Wakhungu, na mkurugenzi wa mamlaka ya bandari (KPA) Gichiri Ndua.

Comments

comments