Wanajeshi zaidi wa KDF watumwa Somalia kupigana na Al-shabaab

Wanajeshi zaidi wa KDF watumwa Somalia kupigana na Al-shabaab

by -
0 558

Serikali inasema itatuma wanajeshi zaidi wa KDF nchini Somalia kukabiliana na Al-shabaab katika ngome zao na kukomboa zana za kivita zilizoibwa katika shambulizi eneo la El adde ambapo wanajeshi kadhaa waliuawa.

Wanajeshi wanaendelea kushambulia kambi za Al-shabaab nchini Somalia huku jeshi likitangaza kumwua kiongozi mmoja wa Al-shabab.

Wakati huo huo familia moja eneo la Likoni hapa Mombasa inaitaka serikali kuharakisha shughuli za kutambua miili ya wanajeshi waliouawa huko Somalia.

Hii ni baada ya familia hiyo kubaini kuwa moja kati ya miili ya wanajeshi waliosafirishwa kutoka Somalia ni ya mwanao ambaye aliaua katika uvamizi huo.

Marehemu Juma Zaro Juma alikuwa miongoni mwa wanajeshi waliouawa Somalia huku serikali ikiwa haijaweka wazi idadi kamili ya wanajeshi waliofariki

Comments

comments