“Matapeli” Wa Pesa Bandia Wanyimwa Dhamana

“Matapeli” Wa Pesa Bandia Wanyimwa Dhamana

by -
0 464

Pesa bandia zilizonaswa ni zaidi ya shilingi bilioni 100,na serikali ya Comoro pia ililalamikia utapeli.

Watu wawili raia kutoka mataifa ya Afrika magharibi wanaodaiwa kupatikana na pesa bandia mjini Nairobi, sasa wanazuiwa korokoroni eneo la Nairobi.

Wanaume hao Ijumaa iliyopita walishtakiwa katika mahakama moja ya Nairobi lakini wakanyimwa dhamana.

Mohamed Hisani anayejiita Daktari Bako  raia wa Niger, pamoja na  Ousman Ibrahim raia wa Cameroon walikana mashtaka mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani -Daniel Ogembo.

Mashtaka yanayowakabili ni kupatikana na pesa-bandia na karatasi za Dola milioni 693 na Euro milioni 369, pamoja na vifaa vya kutengeneza pesa, ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kinyume na sheria.

Iwapo wangefaulu kubadilisha makaratasi hayo basi wangelipata pesa za Kenya zaidi ya shilling billion 100 kwa njia ya utapeli.

Comments

comments