Mgombea wa chama cha Jubilee Malindi apewa cheti

Mgombea wa chama cha Jubilee Malindi apewa cheti

by -
0 322

Chama cha Jubilee kimewapa wagombeaji wao wa ubunge Malindi na useneta Kericho vyeti rasmi vya uteuzi.

Wagombeaji hao ni Philip Charo wa Malindi na Aaron Cheruiyot wa Kericho.

Wasimamazi wa chama hicho JohnStone Sakajja na Prof Kithure Kindiki wanasema wameridhia uteuzi wa wawili hao.

Nacho chama cha ODM kitapeana cheti kwa mgombeaji wake wa Malindi Willy Mtengo.

Viti hivyo viliachwa wazi baada ya rais Uhuru Kenyatta kuwateua Dan Kazungu na Charles Keter mawaziri.

Uchaguzi huu mdogo utafanyika machi 7.

Comments

comments