Kadu-Asili “Kushinda” Ubunge Malindi

Kadu-Asili “Kushinda” Ubunge Malindi

by -
0 517
Mwanasheria kutoka Kilifi Gunga Mwinga ambaye ni mbunge wa Kaloleni.

Mchakato wa kumtafuta mbunge mpya wa Malindi umechacha huku vyama tofauti vikisimamisha wagombea wao, kando na Jubilee na CORD.

Chama cha KADU ASILI kimeamua kuondoa dhana ya kuwa na “vyama vikuu” viwili nchini, na kumtangaza mgombea atakayepeperusha bendera katika uchaguzi mdogo wa Malindi mapema mwezi Machi.

Chama hicho kimekamilisha zoezi la kuwapiga msasa walionuia kusimama, na hatimaye kumteua Rebeun Mwamure kugombea kiti cha ubunge eneo hilo la Malindi.

Uteuzi wake umetanagzwa na mwenyekiti wa kitaifa wa Kadu-Asili Gunga Mwinga, ambaye pia ni mbunge wa Kaloleni aliyechaguliwa kupitia tiketi ya chama hicho.

Bwana Mwinga ambaye ni mwanasheria amehimiza wananchi kudumisha amani wakati wa kampeni za uchauzi mdogo, kwa ajili ya kumchagua mbunge mpya wa Malindi.

Pia ameelezea matumaini makubwa kwa chama chao Kadu-Asili kunyakua ushindi katika uchaguzi huo mdogo uaotarajiwa kuwa na msisimko.

Wakati Reuben Mwamure akipeperusha bendera ya Kadu-Asili atapambana na Fuad Kombe wa New Kanu, William Mtengo wa CORD, na Philip Charo wa JAP (Jubilee) miongoni mwa wagombea wengine.

Mwishoni mwa mwaka jana rais Uhuru Kenyatta alimteua Dan Kazungu aliyekuwa mbunge wa Malindi, katika baraza la mawaziri na hivyo tume ya uchaguzi nchini ikatwikwa jikumu la kuandaa uchaguzi wa ubunge ili kujaza pengo hilo.

~~~~~~~~~~~~~~~ taarifa zaidi imeandaliwa na josephat kioko ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES