Washukiwa wa ulanguzi wa pembe za wanyama pori hatimaye waachiliwa kwa dhamana

Washukiwa wa ulanguzi wa pembe za wanyama pori hatimaye waachiliwa kwa dhamana

by -
0 283

Mahakama ya Mombasa imewaachilia kwa dhamana ya shilingi milioni 10 washukiwa wawili wa ulanguzi wa pembe za wanyama pori.

Hakimu Diana Mochache pia amewaagiza wawasilishe mdhamini sawia na kiasi hicho na kuwataka waripoti kwa afisa wa upelelezi wa kesi hiyo mara moja kwa wiki.

Mochache anasema upande wa mashtaka ulikosa kuwasilisha sababu za kutosha za kuwanyima dhamana.

Ameongeza kuwa upande huo pia ulikosa kuwasilisha sababu zinazoonyesha kuwa washukiwa hao wangekwepa dhamana.

Ali Omar Haji na Said Alfani Mwinyi wanadaiwa kupatikana na pembe za kifaru zenye thamani ya shilingi milioni 3.

Walidaiwa kupatikana wakiuza pembe hizo eneo la Mama Ngina hapa Mombasa, disemba mwaka jana.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES