Kesi ya uchochezi dhidi ya Aladwa yahairishwa

Kesi ya uchochezi dhidi ya Aladwa yahairishwa

by -
0 252

Kesi dhidi ya aliyekuwa Meya wa Nairobi George Aladwa kuhusiana na uchochezi sasa itasikilizwa tarehe 19 na 20 mwezi Aprili.

Hii ni baada ya wakili wake kusema kuwa atakuwepo na shughuli nyingi kabla ya wakati huo.

Aladwa anatuhumiwa kwa kutamka semi za uchochezi wakati wa Mashujaa Day, akiwa eneo la Kibera jijini Nairobi.

Hapo awali , Aladwa alimwahidi hakimu mkuu Daniel Ogembo kuwa hatawashawishi mashahidi.

Mwanasiasa mwingine anayekabiliwa na kesi kama hiyo mahakamani ni mbunge Moses Kuria.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES