Polisi Wanasa Wawili Na Pesa Bandia Shilingi Billioni 100!!

Polisi Wanasa Wawili Na Pesa Bandia Shilingi Billioni 100!!

by -
0 589
Matapeli wasambaza pesa bandia katika miji ya Kenya.

Maafisa wa usalama mjini Nairobi wanawazuia watu wawili raia kutoka mataifa ya Afrika Magharibi, wanaoshukiwa kuwa matapeli wa kimataifa.

Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya Joseph Boinnet anasema wanaume hao -Ousman Ibrahim Bako raia wa Cameroon na Mohammed Sani maarufu kwa jina Dr. Mustafa kutoka Niger, walinaswa mwishoni mwa wiki wakiwa na mabilioni ya pesa bandia.

Mmoja alikamatwa katika mtaa wa Diamond ulio katika Mombasa Road  na mwenzake akatiwa mbaroni katika Kilimani Estate.

Katika mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya idara ya ujasusi mjini Nairobi, Boinnet alisema Jumatatu kuwa washukiwa walinaswa wakiwa na dolla bandia za Marekani millioni 693, na Euro bandia millioni 369.

Hii ina maana kuwa endapo pesa hizo bandia zingebadilishwa zote, basi washukiwa hao wangekuwa na zaidi ya shilingi za Kenya zaidi ya billion 100.

Polisi waliwaandama wanaume hao baada ya kupashwa habari na raia wenye nia nzuri, kufuatia kisa cha wao kutaka kubadilisha Euro na mkazi mmoja wa Nairobi.

Vingine vilivyonaswa katika maskani za watu hao ni pamoja na mitambo ya kuchapisha pesa  bandia, sanduki za kuhifadhi pesa, tarakilishi mbili, wino, makaratasi na kemikali aina tofauti.

Idara ya ujasusi Kenya imedhibitisha kuwa serikali ya visiwa vya Comorro ilikuwa imewasiliana na Kenya, kuhusu kadhaa raia wa kigeni wanaoishi Nairobi na kuendesha mtandao wa matapeli kuwalaghai watu pesa.

Comments

comments