Mwimbaji Wa Injili Marie Misamu Afariki Congo!

Mwimbaji Wa Injili Marie Misamu Afariki Congo!

by -
0 953
Msanii wa injili Marie Misamu afariki akiwa na umri wa miaka 40!

Mashabiki wa muziki wa Injili Afrika Mashariki na eneo la Maziwa makuu wanaomboleza kifo cha mwimbaji nyota wa injili kutoka jamhuri ya Kidemokrasia  Congo, Marie Misamu aliyefariki dunia Jumapili.

Bi Marie aliugua kwa muda mfupi kabla ya kukumbana na mauti yake wakati akitibiwa, baada ya kuhudhuria maombi mwishoni mwa wiki.

Taarifa iliyotolewa na familia yake kupitia binti yake kwa jina la Ruth Misamu, ilisema kuwa msanii huyo (mamake) aliyekuwa na umri wa miaka 40 aliugua na pumu (asthma) iliyokuwa ikimlemea mara kwa mara.

Nyimbo zake za injili ziliibuka kupendwa sana katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki na kati, kama vile kibao kwa jina MASOLO YA KATI

Comments

comments