Hatima ya afisa wa polisi aliyehusishwa na mauaji kujulikana Jumatano

Hatima ya afisa wa polisi aliyehusishwa na mauaji kujulikana Jumatano

by -
0 288

Afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma itatoa mwelekeo siku ya jumatano endapo afisa wa polisi aliyehusishwa na mauaji ya watu 3 ataondolewa mashtaka ya mauaji bila kukusudia au kumfunguliwa mashtaka ya mauaji .

Hakimu Diana Mochache ametoa mwelekeo huo baada ya kesi hiyo kukosa kuendelea kwa muda mrefu kwa madai ya ‘file’ hiyo kutoweka.

Mwezi Novemba mwaka jana hakimu Mochachealifutilia mbali dhamana ya shilingi milioni 2 aliyopewa afisa huyo kwa madai ya kukosa kufika mahakamani.

Harrison Langat anadaiwa kumuua afisa mwenzake wa polisi kwa jina Jacob Nderi pamoja na Dorine Wawira na Alice Kitonye,mwezi machi mwaka wa 2003 katika kituo cha polisi cha Mtwapa.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES