Ukaguzi Katika Magari Ya Uchukuzi Wa Umma.

Ukaguzi Katika Magari Ya Uchukuzi Wa Umma.

by -
0 421
Waandishi wa habari mjini Mombasa wakichunguza usalama katika magari ya Umma kama vile Tuk-tuk.

 

Idara ya Polisi nchini Kenya iliagiza Ijumaa ukaguzi wa kina ufanyiwe raia na wageni kote nchini, kufuatia matukio mapya ya mashambulio ya kigaidi.

Inspekta mkuu wa Polisi Joseph Boinnet ameamuru walinda-usalama na walinzi wa kibinafsi kuwakagua watu wanaotembelea majumba mijini, na hata abiria katika magari ya uchukuzi wa Umma.

Hivi majuzi wahudumu wa Tuk-tuk mjini Mombasa walipinga pendekezo la kuwaondoa kati-kati mwa jiji wanakohudumu, baada ya kudaiwa wanahusika na ongezeko la uhalifu.

Agizo hilo lilitolewa Ijumaa asubuhi katika siku ambapo magaidi walishambulia nchi za Somalia na Indonesia na kuwaua watu wengi.

Waliouawa karibu na mpaka wa Kenya na Somalia ni pamoja na wanajeshi wa Kenya (KDF) wanaohudumu katika majeshi ya muungano nchini Somalia.

Wanamgambo wa Al Shabaab walikiri kuhusika na shambulio hilo, kukiwa na habari za kuhitilafiana kuhusu idadi ya wahanga.

Comments

comments