Nilimwamini Feisal Mohammed Kwa Misingi Ya Kidini –Asema Shahidi.

Nilimwamini Feisal Mohammed Kwa Misingi Ya Kidini –Asema Shahidi.

by -
0 371
Abdulrazak Omar -shahidi katika kesi ya ulanguzi wa pembe za ndovu Mombasa.

 

Mfanyabiashara mmoja wa Mombasa anasema familia yake imeteseka kwa miezi mitano sasa tangu gari lake liliponaswa na polisi wa kitego cha ujausu, kwa kuhusishwa na usafirishaji wa pembe za ndovu kati kati ya mwaka wa 2014.

Abdulrazak Omar Abdallah alikamatwa na majasusi Agosti mwaka 2015 baada ya kupigiwa simu na maafisa wa upeleelzi, waliojitambulisha kama wateja waliotaka kubebewa mizigo.

Anasema tangu wakati huo gari lake aina ya Mitsubishi Canter lenye nambari za usajili KAM 832 W ambalo alilinunua kwa bei ya shilingi milioni 1.2 miaka minnne iliyopita, linazuiliwa na polisi kama ushahidi.

Abdulrazak aliambia mahakama kuwa alijihisi kusalitiwa baada ya gari lake kunaswa na polisi wa kitengo cha upelelezi, kwa kuhusishwa na biashara ya ulanguzi wa pembe za ndovu.

Yeye ni miongoni mwa mashahidi 22 ambao wameitwa kuhojiwa katika kikao maalum cha mahakama ndani ya kambi ya shirika KWS eneo la Bamburi hapa Mombasa.

Abdulrazak anasema alimwamini Feisal kutokana na imani yake ya kidini kwa kusali msikiti mmoja mjini Mombasa, akiwa na tumaini kuwa gari lake litarejeshwa salama.

“Kweli shetani hafuati mlevi,pepo yuko na anakujia kupitia kwa mtu mwungwana”, alisema Abdulrazak, mmiliki wa gari analosema alimkodoshia Feisal Mohammed.

Feisal Mohamed pamoja na washukiwa wengine 5 walidaiwa kulangua pembe za ndovu vipande 314 vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi million 44 zilizonaswa katika bohari moja katika kampuni ya magari ya Fuji Motors East Afrika eneo la Tudor mjini Mombasa, Juni mwaka 2014.

Comments

comments