Afisa wa polisi auawa kwa kupigwa risasi Likoni

Afisa wa polisi auawa kwa kupigwa risasi Likoni

by -
0 505

Afisa wa polisi ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko Likoni katika kisa cha wizi.

Inasemekana majambazi hao watatu walimpiga risasi afisa huyo kabla ya kutoroka na bunduki yake aina ya G3.

Afisa huyo alikuwa akitoa ulinzi kwa lori la kubeba unga na bidhaa zingine za duka la Mombasa mazie millers.

Majambazi hao waliokuwa kwenye pikipiki walitoroka na shilingi elfu 42 pesa taslim.

Dereva wa lori hilo Abdula Aziz na utingo wake Mwinyi Ali aliambika Baraka FM kuwa majambazi hao walikuwa wakiwaandama.

Comments

comments