Wanawake kujiunga na makundi haramu Kilifi yazua wasiwasi

Wanawake kujiunga na makundi haramu Kilifi yazua wasiwasi

by -
0 554

Kamishena wa kaunti ya Kilifi Joseph Keter amewaonya wanawake na vijana dhidi ya kujihusisha na makundi haramu katika kaunti hiyo.

Badala yake Keter amesema wanawake na vijana wanaweza kujiunga na  makundi ya maendeleo kupitia hazina ya CDF ambayo hatimaye itawasaidia kuimarika kiuchumi.

Keter amesema kuwa kama viongozi wataweka mikakati ya kuleta maendeleo kwa vijana na wanawake.

Haya yanajiri siku chache baada ya Kamishena huyo wa kaunti kufichwa kuwa wanawake ndio wanajiunga kwa wingi na kundi haramu la MRC huko Kilifi.

Hivi majuzi washukiwa 17 wanaoaminika kuwa wafuasi wa MRC walikamatwa huko chonyi MWARAKAYA na JIBANA ambapo wawili kati yao walikuwa wanawake.

Comments

comments