Mtanzania Samatta Ashinda Tuzo Ya CAF.

Mtanzania Samatta Ashinda Tuzo Ya CAF.

by -
0 405
Mshambuliaji wa Gabon Aubameyang aliyeshinda tuzo ya CAF.

Mchezaji kutoka Tanzania ametuzwa miongoni mwa wanasoka bora zaidi barani Afrika, mwaka ulipkamilika wa 2014.

Mbwana Aly Samatta ndiye mwanasoka bora wa shiriksiho la CAF, kitengo cha wachezaji walio katika ligi za mataifa ya Afrika.

Samatta anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Congo alituzwa jana usiku katika hafla iliyokuwa katika mji wa Abuja nchini Nigeria.

Naye mwanasoka bora zaidi ni mshambuliaji wa Gabon – Pierre-Emerick Aubameyang, kwa kuwapiku wanasoka wengine waliokuwa wameteuliwa -Yaya Toure wa Ivory Coast na Andre Ayew kutoka Ghana.

Aubemeyang anayechezea Borrusia Dortmund ya Ujerumani alipata kura 143, Toure akapata kura 136, naye Ayew akapata kura 112.
Washindi walipatikana kupitia kura iliyopigwa na makocha na wakurugenzi wa kiufundi, kutoka mataifa wanachama wa CAF.

Mwanasoka bora wa kike ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon.

Kocha bora barani Afrika ni Herve Renard aliyeongoza Ivory Coast kutwaa “Africa Cup Of Nations” mwaka jana wa 2015.
Renard pia aliongoza “Chipoloolo” ya Zambia kushinda kombe hilo mwaka 2012.

Klabu ya TP Mazembe ambayo Disemba mwaka jana ilishiriki katika dimba la FIFA la klabu bingwa duniani imeteuliwa kama timu bora zaidi barani Afrika.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES