Imam ahukumiwa jela miaka 20 kwa kuwafunza wanafunzi itikadi kali

Imam ahukumiwa jela miaka 20 kwa kuwafunza wanafunzi itikadi kali

by -
0 356

Mahakama ya Mombasa imemhukumu kifungo cha miaka 20 gerezani mwalimu wa dini aliyepatikana na hatia ya kutoa mafunzo ya itikadi kali.

Salim Muhamud Wabwile ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, alishtakiwa mwaka 2014 kwa madai ya kutoa mafunzo ya itikadi kali, katika msikiti wa Gotani huko Kaloleni kaunti ya Kilifi.

Hakimu wa Mombasa Diana Mochache alisema upande wa mashtaka umethibitisha kuwa mshukiwa alitoa mafunzo hayo kwa wanafunzi kwa shule ya msingi.

Awali mwanafunzi mmoja aliambia mahakama kuwa mwalimu huyo aliandika majina ya “Radical” kwa shati zao, licha ya Imam huyo kukana shtaka hilo.

Hata hivyo mahakama ilimwondolea mashtaka mengine mawili likiwemo la kuwa mwanachama wa Al-shaabab, na kusajili wanafunzi katika kundi hilo.

Amepewa siku 14 za kukata rufaa.

Comments

comments