Matamshi ya Shahbal yazidi kumtia taabani

Matamshi ya Shahbal yazidi kumtia taabani

by -
0 690
Suleiman Shahbal , Mombasa Politician com Jubilee Alliance Party official.

Mwanasiasa wa Mombasa Suleiman Shahbal anaendelea kujipata matatani kufuatia matamshi yake yanayodaiwa kuwa ya uchochezi.

Sasa mkurugenzi wa mashtaka  Keriako Tobiko amwagiza mkurugenzi wa CID kumchunguza kuhusu matamshi aliyotoa hapo wikendi akiwa kwenye kampeni za kupigia debe chama cha Jubilee huko Malindi kaunti ya Kilifi.

Shahbal alinukuliwa akisema kuwa Jubilee itashinda uchaguzi mkuu ujao kwa mbinu zote ikiwemo kuiba kura na hata kuwanunua wapiga kura.Tobiko amesema  kuwa matamshi ya Shahbal ni ya uchochezo na iwapo mkurugenzi wa CID na atampata na hatia,basi huenda akafunguliwa mashtaka.

“Basi mara hii nawambia, uchaguzi wa 2017 tutashinda, tutashinda kwa nguvu, tutanunua, tutaiba whatever will be” alisema Shahbal alipozungumza hadharani katika mkutano huko Malindi.

Shahbal aliwania kiti cha ugavana wa Mombasa bila mafanikio  kwenye uchaguzi wa 2013 kupitia tiketi ya chama cha Wiper kabla ya kuhamia mrengo wa Jubilee hivi majuzi.

Hapo Jumanne , Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi, alikosoa matamshi  hayo ya Suleiman Shahbal huku akimtaka achukuliwe hatua ya kisheria.

Akizungumza na wanahabari ofisini mwake Gavana Kingi alitaja matamshi hayo kuwa yasiyofaa na akaahidi kuwasilisha kanda ya video ya shahbal aliponukuliwa akisema matamshi hayo kwa idara husika ili hatua za kisheria zichukulie dhidi yake.

Amesema mrengo huo umejipanga kikamilifu kukabiliana na visa kama hivyo.

Comments

comments