Mahakama yaagiza kuchunguzwa mshukiwa wa Alshaabab

Mahakama yaagiza kuchunguzwa mshukiwa wa Alshaabab

by -
0 335

Mahakama ya Mombasa imeipa polisi siku 30 kuchunguza mwanamume mmoja anayehusishwa kuwa gaidi.

Hakimu Diana Mochache ametoa mwelekeo huo kufuatia ombi lililowasilishwa mahakamani na wakili kutoka ofisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma Lidya Kagori.

Kagori ameiambia mahakama kuwa mshukiwa Mahmoud Salim Mohamed ni miongoni mwa washukiwa wa ugaidi waliotoweka eneo la Kingorani katika nyumba iliyopatiakana na bunduki,risasi na nyaya za kutengeneza vilipuzi.

Kagori ameongeza kuwa mshukiwa Mahmoud anakisiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Alshabab, na anauhusiano wa karibu na washukiwa wengine ambao bado wanasakwa.

Mshukiwa alikamatwa hapo jana na maafisa wa CID katika kituo cha polisi cha Malindi kaunti ya Kilifi.

Mshukiwa ataendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilindini huku kesi hiyo ikiratibiwa kutajwa mwezi februari.

Comments

comments