Sherehe za mwaka mpya zatajwa kama ubadhirifu wa fedha-Taita Taveta

Sherehe za mwaka mpya zatajwa kama ubadhirifu wa fedha-Taita Taveta

by -
0 436

Baadhi ya wakaazi katika kaunti ya Taita Taveta wameikosoa serikali ya kaunti kwa kuandaa kesha ya mwaka mpya hapo jana na kulitaja swala hilo kama ufujaji wa fedha za umma.

“Bado sisi tuna njaa watu wanashida kaunti hii hizo pesa karibu milioni tatu za kaunti zingetumiwa kufanya maendeleo hapa,” alisema Bwana John Mwangeka;mkaazi wa Taveta.

Kulingana na mmoja wa wakaazi sherehe hizo ambazo zilifanyika katika uwanja wa moi mjini voi,ni kuharibu fedha za wananchi pamoja kuchangia utovu wa nidhamu kama vile ukahaba miongoni mwa vijana.

Sherehe hizo zilihusisha waimbaji tofauti kutoka Tanzania na wakutoka kaunti hiyo Lakini kinachowakera zaidi wakaazi wa kaunti hiyo ni kuwa baadhi ya wasanii waalikwa hawakuja huku wengine wakidai kuwa huenda ilikuwa njia moja ya kutumia vibaya pesa za mwananchi.

“Hata waimbaji wetu wa Taita  bado hawajahusishwa sana waenda chukua waimbaji wa tanzania ni kitu gani tunajivunia kutoka kwao,” aliongezea Bwana Mwangeka.

Comments

comments