Sita Wanaswa Watamu Kuhusiana Na Mauaji Ya Mtalii Daktari.

Sita Wanaswa Watamu Kuhusiana Na Mauaji Ya Mtalii Daktari.

by -
0 303

Watu sita wamekamatwa na polisi wilayani Malindi kuhusiana na mauaji ya mtalii mmoja raia wa Italy, aliyeuawa Jumamosi usiku mjini Watamu.

Watu wengine kadhaa akiwepo mzazi wa mtalii huyo wa kike walijeruhiwa katika tukio hilo la uvamizi, pale nyumba yao ilipovunjwa usiku huo.

Waziri wa usalama wa ndani nchini Joseph Nkaiserry ambaye Jumatatu jioni aliziri Watamu, amesema jukumu la kulinda usalama ni la kila mkenya kwa kuhakikisha anapiga ripoti kwa maafisa wa usalama.

Nkaissery amesema serikali kuu imeweka mikakati ya kuhakikisha usalama unadumishwa kote nchini.

Nkaissery amedhibitisha kuwa mshukiwa aliyekamatwa kwanza anasaidia polisi kuwasaka wahusika wa shambulio hilo la kikatili.

Katika ziara hiyo mjini Watamu waziri Nkaissery aliandamana na Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinnet, pamoja na maafisa wengine waandamizi katika vitengo vya usalama.

Comments

comments