Lamu Yavutia Watalii Wengi Zaidi

Lamu Yavutia Watalii Wengi Zaidi

by -
0 333

Utawala kaunti ya Lamu umehakikishia watalii na waekezaji wengine usalama wakati wowote wanapokuwa katika shughuli zao huko Lamu na visiwa vyote eneo hilo.

Kamishna wa kaunti ya Lamu Fredrick Ndambuki ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usalama kaunti hiyo, alisema Jumapili kuwa vikosi vyote vya usalama vimeungana na hata kufanikisha zoezi la kiusalama ndani ya msitu wa Boni.

Ndambuki alidokeza hilo wakati wa sherehe za kila mwaka za utamaduni wa Lamu, zilizokamilika rasmi Jumapili iliyopita.

Naye waziri mpya wa utalii aliyeteuliwa juma lililopita -Najib Balala aliahidi kusaidia kufufua tena sekta ya utalii nchini.

Balala anasema uchumi wa taifa umeathirika na shilingi ya Kenya kushuka thamani kutokana na mmiminiko wa kiwango cha chini wa fedha za kigeni humu nchini.

Wageni wangi ambao walihudhuria sherehe za mwaka huu za utamaduni wa Lamu wameripotiwa kuinua kwa kiwango kikubwa biashara eneo hilo.

Zaidi wa wageni 20,000 kutoka nchini na mataifa ya nje walifurika kwa sherehe ya 15 ya utamaduni huo ambao hupokea maelfu ya watu kila mwaka.

Sherehe za utamaduni wa watu wa Lamu zilizinduliwa rasmi mwaka 2001.

Comments

comments