Harambee Stars Yatinga Robo-Fainali Kutetea CECAFA.

Harambee Stars Yatinga Robo-Fainali Kutetea CECAFA.

by -
0 449

Timu ya taifa Harambee Stars inajiandaa kucheza na Rwanda katika mchuano wa robo-fainali kombe la Cecafa Senior Challenge, baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Michuano hiyo ya kandanda inaendelea nchini Ethiopia, na Kenya ni miongoni mwa tim 8 zilizofuzu kwa hatua ya robo-fainali.

Licha ya kuchapwa na Zanzibar mabao 3-1 katika mechi ya kundi la B, Kenya ilifuzu Jumamosi jioni baada ya Uganda Cranes kulaza Burundi bao 1-0 hivyo Kenya ikamaliza ya pili nyumma ya Uganda.

Zanzibar ilikuwa haijashinda Kenya tangu mwaka wa 1980.

Harambee Stars sasa itakutana na Rwanda katika mchuano wa robo-fanali, Disemba tarehe moja mjini Addis Ababa.

Kocha mkuu Bobby Williamson atalazimika kuwa makini zaidi kwa kuepuka kosa alilotenda kabla ya kucheza na Zanzibar, alipowabadilidha wachezaji saba kutoka kikosi cha kwanza, na kuishia kufedheheshwa na Zanzibar.

Comments

comments